Shirika hilo,Foundation for Environmental Protection in Tanzania (FEPT),limezindua upandaji wa miti 5000 katika kata hiyo, ikiwa ni awamu ya kwanza ya kuuunga mkono jitihada za kuifanya Arusha kuwa kijani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hizo jana na ugawaji na upandaji wa miti, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Peter Mhagama alisema wameanza na zoezi hilo kwenye kata hiyo baada ya kuona eneo kubwa lipo wazi.
Alisema maeneo waliotoa kupaumbele kwenye upandaji miti hiyo katika kata ya Murriet ni kwenye shule za sekondari na msingi za serikali, zahanati,vituo vya afya na ofisi za serikali ya mtaa yote ya kata hiyo.
“Hili zoezi ni shirikishi na ndio maana tnawagawia wananchi miti ili kila mmoja akapande nyumbani kwake na kuitunza tukiamini ili mwisho wa siku Arusha yetu iwe ya kijani,” alisema.
Aliongeza kuwa mipango ya FEPT ni kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wanafanikiwa kutimiza malengo yao ya kuifanya Arusha iwe ya kijani kwa kupanda miti katika kata zote zenye upungufu wa miti na hivyo kulipendezesha jiji la Arusha
Mkurugenzi Mtendaji huyo aliushukuru Ubalozi wa Canada nchini kwa kuunga mkono kampeni hiyo na kuwataka wadau wengine wajitokeze kuunga mkono kampeni hiyo muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri maisha ya watu kila siku.
Afisa Tarafa ya Elerai Tito Cholobi aliomba shirika hilo kujikita kwenye ugawaji miti mitano kwa kila familiya kila mwaka ili kutimiza lengo lao la kugeuza Arusha ya kijani.
Aliomba kila mdau wa mazingira kuhakikisha miti inayopandwa ianatunzwa ili lengo la kupendezesha Arusha litimie.
“Nawaomba wananchi pandeni miti kwa wingi sababu miti ni mtaji mzuri hata ukipanda baada ya miaka miatatu au minne unabadilika na kukuletea fedha lakini ineta hewa nzuri na kuboresha mazingira,”alisema.
Diwani wa Murriet, Francis Mbise alisema miti hiyo imepelekwa wakati muafaka na kipindi cha mvua na kushukuru kwa msaada huo, ambao utabadilisha mazingira yao ambayo nyumba nyingi zipo wazi sababu ya ukosefu wa miti hasa maeneo ya mlimani.